MCHANGO WA MAZINGIRA YA MWANDISHI KATIKA MATUMIZI YA MAFUMBO

AYIERA Elijah Arasa, ONTIERI James Omari, AYODI Nancy

Abstract


Lugha ni kiungo muhimu cha riwaya kwani ni kupitia kwa lugha ambapo mwandishi huyafikia malengo yake ya kisanaa na kuwasilisha ujumbe wake. Suala hili limechangamkiwa na watafiti wengi wa fasihi kote ulimwenguni. Makala hii inajikita katika kuchunguza mchango wa mazingira ya mwandishi katika matumizi ya mafumbo kwenye riwaya mbili za Katama Mkangi: Mafuta na Walenisi. Kwanza, makala hii imebainisha kuwa, wakati ambapo Mkangi alikuwa akiandika riwaya hizi, uhuru wa kuikosoa serikali iliyokuwa mamlakani haukuwepo na kwa hivyo, alilazimika kutumia ufumbaji kuwasilisha ujumbe wake ili kuhepa rungu ya serikali. Pili, alikosomea na waandishi wengine, walimwathiri katika matumizi ya mbinu ya ufumbaji katika Uandishi wake. Tatu, hali ya kisiasa dhidi ya waandishi wakati wa uandishi wake ilimlazimisha kutumia lugha ya ufumbaji ili ichukuane na wakati huo. Aidha, kutokana na makala hii ni dhahiri kuwa Mkangi alitumia mbinu ya ufumbaji kumzindua msomaji kuhusu athari za utabaka, ubepari, unafiki wa viongozi miongoni mwa mengine. Yaliyoshughulikiwa katika makala hii yalilikusanywa kupitia kwa upekuzi wa maandishi na riwaya mbili za Mkangi: Mafuta na Walenisi kwa kuzingatia lugha ya mafumbo. Makala haya ni muhimu kwa kuwa yatawasaidia wasomaji kuelewa kazi hizi za Mkangi zilizoandikwa kimafumbo.

Full Text:

PDF

References


Mkangi, K. G. C. (1984). Mafuta. Nairobi: East African Educational Publishers.

Mkangi, K. G. C. (1994). Walenisi. Nairobi: East African Educational Publishers.

Momanyi, J. (1991). Matumizi ya Taswira Kama Kielelezo cha Uhalisi katika Utenzi wa Al-Inkishafi. Tasnifu ya M.A, Chuo Kikuu cha Nairobi (Isiyochapishwa).

Msokile, N. (1993). Msingi wa Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: East African Educational Publishers.

Musembi, N. N. (2005). Matumizi ya Taswira na Ukinzano Katika Riwaya za Mkangi. Tasnifu ya M.A, Chuo Kikuu cha Kenyatta (Isiyochapishwa).

Mwenda, N. (2004). Uhakiki wa Kazi za Fasihi. Rock Island: Augustana Collage.

Ogot, B. A. na Ochieng’, W. R. (1995). Decolonization and Independence in 1940 – 1993. Nairobi: East African Educational Publishers.

Vunyoli, A. J. (2004). Hadith Kama Chombo cha Maudhui Katika Riwaya za Mkangi. Tasnifu ya M.A, Chuo Kikuu Cha Kenyatta (Isiyochapishwa).

Wamitila, K. W. (1988). Towards Unlocking Katama Mkangi’s Walenisi. A case Study of Parabolic Narrative Katika Kiswahili Juzuu 61, 1999. Dar es Salaam: TUKI.

Wamitila, K. W. (2004). Kichocheo cha Fasihi: Simulizi na Andishi. Nairobi: Focus Publications Ltd.


Refbacks

  • There are currently no refbacks.