MAKOSA YA KISEMANTIKI KATIKA MAWASILIANO ANDISHI YA KISWAHILI YA WANAFUNZI WA SHULE ZA UPILI NCHINI KENYA

ARUBA Beatrice Kemunto, MOHOCHI Sangai Ernest, ONTIERI James Omari

Abstract


Lugha ni kipengele muhimu ambacho huwezesha kuwepo kwa mawasiliano miongoni mwa watu. Katika juhudi za kurahisisha uwasilishaji na upokeaji wa ujumbe, ni muhimu kuhakikisha kuwa lugha sahihi imetumiwa. Katika karne hii ya 21 ya mawasiliano ya sayansi na teknolojia, suala la mawasiliano limeshika kasi kubwa kwa kila mtu. Kwa namna hii mawasiliano yamekuwa ni jambo muhimu sana ambalo humwezesha mtu kupashana habari, taifa kutoa taarifa mbalimbali kwa wananchi kuhusu matukio, na hata malengo na mikakati iliyojiwekea. Iwapo makosa yatatokea katika maandishi au mazungumzo, mawasiliano kama shughuli kuu ya kibinadamu hayatafaulu. Madhumuni ya makala haya ni kuchanganua makosa ya kisemantiki yanayojitokeza katika mawasiliano andishi ya Kiswahili ya wanafunzi wa shule za upili. Makala haya yametumia nadharia ya Uchanganuzi Makosa (Corder, 1967) kuonyesha kuwa wanafunzi wanaojifunza lugha ya pili hufanya makosa ambayo yanaweza kubainishwa, kuchanganuliwa, kuainishwa na kutathminiwa ili kubainisha mfumo unaofanya kazi. Data ya makala haya ilikusanywa kutoka kwa wanafunzi wa shule za upili hususani kidato cha tatu, kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Mbinu iliyotumiwa katika ukusanyaji wa data ni ya nyanjani (hojaji na mjarabu). Katika kubainisha makosa husika, makala haya yametumia vielelezo mbalimbali kutoka kwa watafitiwa lengwa. Makala haya pia yanatoa mapendekezo ya utatuzi wa makosa yanayojitokeza katika matini za wanafunzi wa shule za upili. Makala haya yatawafaidi walimu wa Kiswahili, wanafunzi wa shule za upili na vyuo vya elimu ya juu katika kurekebisha makosa ya kisemantiki katika matini anuwai.


Full Text:

PDF

References


Asiba, A.(1995, August 30). Can Sheng Stand the Test of Time. Sunday Nation Nairobi, p9

Brown, H.D. (1987). Principles of Language LearningAND Teaching. Retrieved May 10, 2014 from http:www.google.com.

Corder, S. P. (1967).The Significance of learners Errors. Reprited in J. C., Richards (Mh) (1974, 1984) Error Analysis: Perspective on second Language Acquistion. London: Longman. Reprited January 12, 2014 From http: absamra 03 Tripod.Com/…/languageacg-erranalysis.htm.

Crowley, T. (1982). An Introduction to Historical Linguistic. Oxford: O.U.P.

Ellis, R. (1994). The Study of Second Language Acquistion. Oxford: Oxford University Press.

Cruse, D. A. (1986).Lexical Semantic.Cambridge: Cmbridge University Press.

Fauconnier, G. (1997). Mapping in Thought and Language. Cambridge: Cambridge University Press.

Griffiths, P. (2006). An Introduction of English Semantic and Pragmatic. Edniburgh: Edniburgh University Press.

Habermas, J. (1979). What is Universal Pragmantics? Trans. Thomas McCathy, Communication and Evolution of Society. BOSTON: Beacon, 1-68.


Refbacks

  • There are currently no refbacks.