KINAYA KATIKA TAMTHILIA YA KISWAHILI: MFANO WA TAMTHILIA YA MSTAHIKI MEYA

FRIDAH Oiko Gesare, James Ontieri Omari, EMMANUEl Kisurulia Simiyu

Abstract


Mwandishi wa kazi ya fasihi kama mzawa wa jamii anayoindikia, huwa na mbinu mbalimbali za kisanaa anazoweza kutumia katika kuwasilisha mawazo yake kama anavyoyashuhudia katika jamii. Mbinu hizi ni nyingi na hivyo mwandishi hulazimika kufanya uchaguzi wa ile itakayofaa ujumbe anaowasilisha. Uchaguzi huu huathiriwa na jinsi anavyotaka mawazo yake kueleweka na kuleta taathira anayokusudia. Aidha mbinu anayoteua mwandishi sharti iwe ni ile isiyotinga mahusiano ya wanajamii (watawala na watawaliwa). Mojawapo ya mbinu hizo ni kinaya. Kinaya ni mbinu ya kisanaa ambayo hulenga kukuza mawazo kwa njia iliyo kinyume na matarajio. Makala haya yametathmini matumizi ya kinaya katika kukejeli viongozi wa nchi changa za Bara la Afrika ambao katika utendaji kazi duni ambao umezalisha maendeleo yasiyokuwepo. Makala haya yameongozwa nadharia ya Uhakiki wa Kimtindo. Makala haya yamebainisha kwamba Arege ameegemea sana mtindo wa kinaya katika kuwasilisha mawazo yake. Imebainika pia kuwa lengo kuu la kinaya ni kusuta kwa lengo la kuadilisha wanajamii katika kuimarisha viwango vya maendeleo yanayohitajika katika katika sekta mbalimbali. Aidha, kupitia kwa makala haya imebainika kuwa Arege ameegemea sana kinaya ili kukejeli jamii nzima bila kuhujumu mahusiano ya kitabaka yaliyomo katika jamii anayoiandikia. Makala haya yamezingatia kinaya kwa kuegemea nadharia ya Uhakiki wa Kimtindo.

Full Text:

PDF

References


Haiman, J. (1990). Sarcasm as theater: Cognitive linguistics, 1(2), 183-203.

Ilhan, O. (2001). Role of Education in Economic Development: A Theoretical Perspective. https://mpra.ub.uni.muenchen.de/9023.

Kamusi ya Karne ya Ishirini na Moja (2011). Toleo la pili. Nairobi: Longhorn Publishers.

Kuhenga, C. (1977). Tamathali za Usemi za Kiswahili. Nairobi: East Africa Literature Bureau.

Leech, G. (1969). A linguistic Guide to Modern English Poetry. Essex: Longman Group Ltd.

Leech, G. & Short, M. (2007). Style in Fiction: A Linguistic Introduction to Fictional Prose: New York: Longman Limited.

Mbatiah, M. (2001). Kamusi ya Fasihi. Nairobi: Standard Textbooks Graphics and Publishing Ltd.

Mrikaria, E. S. (2007). Kejeli katika Fasihi ya Kiswahili- Tanzania. Katika Swahili Forum nambari 14, Uk.197-206. Chama cha Masomo ya Kiafrika.

Msokile, M. (1993). Misingi ya Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: East Africa Educational Publishers Ltd.

Mohamed, S.A. (1995). Amezidi. Nairobi: East Africa Educational Publishers.

O.U.P. (2008). The Oxford Advanced Learners English Dictionary. (Toleo la 8). Oxford University Press.

Scaffer, R. R. ( 1982). Vocal Clues for Iron in English. Unpublished Ph.D thesis. University of Oihio State.

Senkoro, F. E.M.K. (2011). Fasihi. Dar es Salaam: KAUTTU Ltd.

Short, M. (1996). Exploring the language of Poems, Plays and Prose. London: Longman Publishers Limited.

Orwell, G. (1988). Shamba la Wanyama. Nairobi: Phoenix Publishers.

Wales, K. (1989). A Dictionary of Stylistics. London: Longman PublishersGroup.

Wales, K. (2001). A Dictionary of Stylistics. United Kingdom. Pearson Education Limited.

Wamitila, K. W. (2002). Uhakiki wa Fasihi: Misingi na vipengele vyake. Nairobi: Phoenix Publishers.

Wamitila, K. W. (2003). Kichocheo cha Fasihi: Simulizi na Andishi. Focus Publications Limited.


Refbacks

  • There are currently no refbacks.